Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano kwenye orodha
ya viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa leo na Shirikisho la soka la
kimataifa FIFA.
Hiyo ina maana kwamba Tanzania sasa imeangukia
katika nafasi ya 130 kwenye viwango hivyo.
Tanzania hawajahesabiwa mechi yoyote ya hivi
karibuni ambapo Taifa Stars ilishinda bao 1-0 dhidi ya Chad katika mechi ya
kwanza ugenini lakini Chad wakajiondoa na hawakushiriki mechi ya marudiano
jijini Dar es Salaam.
CAF ilifuta matokeo hayo dhidi ya Chad katika kundi
G.
Miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Uganda inaongoza ikiwa nafasi ya 72, Rwanda inafuata ikiwa nafasi ya 87, Kenya
nambari 115, Burundi nambari 122 na Tanzania nambari 130
Orodha
ya mataifa tatu bora Afrika ni kama ifuatavyo:
Algeria
Ivory Coast
Ghana

0 comments:
Post a Comment