Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Dokta Jonas
Tiboroha amelamba dili katika klabu ya Stand United ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Stand United, Muhibu
Kanu alisema wameridhishwa na uzoefu na uwezo wa Toboroha pamoja na taaluma
yake kwa ujumla.
Alisema tayari Tiboroha amekubali kufanya nao kazi
hasa baada ya kuafikiana katika masuala mbalimbali ya ajira hiyo.
“Stand sasa inakwenda kuwa kampuni kwa hiyo ili
kuendana na hadhi hiyo tumelazimika kuimarisha sekretarieti kwa kuajiri
wataalamu watakaotusaidia,” alisema Kanu.
Hata hivyo Dokta Tiboroha ameibua maswali kwa wana
Yanga hasa kufuatia kauli aliyoitoa hivi karibuni wakati akiachana na Yanga ya kwamba
anakabiliwa na kazi za Serikali katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, hivyo
hatoweza tena kujihusisha na masuala ya soka kwa sababu yanampunguzia umakini
wa ajira yake ya uhadhiri.
Tiboroha alijiuzulu nafasi yake ya ukatibu ndani ya
Yanga kwa madai ya kutokuwa na maeleano mazuri na Mwenyekiti wa Klabu hiyo
Yusufu Manji, ingawa mwenyewe hakuweka wazi.

0 comments:
Post a Comment