MAMBO SITA YA WAYNE ROONEY KABLA YA KUINGIA UWANJANI




LEO tunamuangalia mshambuliaji wa klabu ya soka ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney ambaye msimu huu makali yake yameonekana kupungua ikilinganisha na miaka ya nyuma.

Hata hivyo mwanandinga huyo bado ni hatari hasa anapopata nafasi katika eneo la hatari la timu pinzani.

Pia imekuwa ni kawaida kwa mchezaji yoyote kujiwekea malengo na ratiba yake kabla ya kucheza mchezo wowote.

Suala hilo lipo kwa Rooney ambaye hujifanyia mandalizi binafsi ya kimwili na kiakili kabla ya kucheza mechi.

Yafuatayo ni mambo sita ambayo Rooney huwa anayazingatia kabla ya kucheza mechi kubwa. 

KULALA
 “Huwa ninajitahidi kupata saa nane za kulala usingizi usiku pamoja na saa moja ama mawili wakati wa mchana.Kufanya mazoezi kwa saa nane ni nzuri”
 “Siwezi kujilaza kitandani na kulazimisha usingizi.Nitasubiri hadi nitakapochoka, kwa kawaida ifikapo saa 5 ama 6 usiku huwa napata usingizi na kisha huamka saa mbili asubuhi”

Unaweza kuona tofauti endapo hautolala kwa muda mrefu, jambo ambalo hutokea baada ya mechi za usiku.Unajikuta siku inayofuata unachoka katika utendaji wako,”alisema.


MAONO
 “Mara zote huwa napenda kuutengenezea picha mchezo usiku mmoja kabla ya mechi.Kwanza huwa ninamfuata mtunza jezi  na kumuuliza jezi ipi tunapaswa tuvae siku hiyo, lengo likiwa ni kuitengenezea picha kichwani mwangu.Ni kitu ambacho mara nyingi hufanya tangu lilipokuwa mdogo”

 “Inasaidia kuweka mawazo wako katika matukio yanayotarajiwa kutokea siku inayofuata”

 “Huwa nafikiri hivyo wakati nikiwa kitandani.Huwa ninajiuliza nitafanya nini endapo mpira wa krosi utakuja kwenye boksi kwa namna hii? Mjongeo gani nitatumia ili kuunganisha krosi hiyo na kufunga?”

Hayo na mengine mengi humfanya Rooney ajiulize ili kazi yake iweze kuwa rahisi ifikapo siku ya mechi.

VYAKULA
 “Usiku mmoja kabla ya mechi huwa nakula kuku, pasta na samaki.Hivyo  ndivyo vyakula tunavyotarajiwa kula wote”

 “Kama ni mechi ya mapema zaidi, unajaribu kula usiku mmoja kabla kwasababu huwezi kula kwa kufakamia muda wa asubuhi”

“Siku ya mechi huwa nakula ndizi kama chakula cha kujiandaa na mchezo”

UTARATIBU
“Wachezaji mara zote hufanya hivi hivi  huku wengine wakifanya tofauti. Huwa ninakwenda kuendesha baiskeli kwa dakika 15 halafu ninajinyoosha na kisha kupumzika”

 “Baadhi ya wachezaji hufanya utaratibu wa aina moja wa maandalizi kila wiki kabla ya kila mechi, lakini binafsi sipendi.Mimi si mshirikina. Huwa ninajaribu kuwa makini na kuzingatia ninachokiamini”

MUZIKI
“Patrice Evra alikuwa anapenda kusikiliza muziki katika vyumba vya kubadilishia nguo. Muziki wa pop ya Kifaransa, kitu kama hicho. Lakini kila mmoja husikiliza. Ni jambo jema tukawa tunasikiliza muziki wote kwa pamoja na si kila mmoja kusikiliza peke yake kwa iPod yake”

SAA LA MWISHO
 “Ninakunywa kinywaji cha kuongeza nguvu(energy drink) dakika 40 kabla ya mchezo kuanza na kisha ninakwenda nje kufanya mazoezi ya viungo ambayo huchukua nusu saa kabla ya mchezo kuanza”

 “Dakika 10 kabla ya mechi kuanza, tunarejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Ninavaa jezi yangu, kilinda ugoko na kisha ninakwenda tena uwanjani”
“Muda huo ni sahihi, lakini saa moja kabla ni jambo baya kama utakaa bila kufanya chochote”
mpanduka@yahoo.com
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment