SIMBA INATIA HURUMA, MAYANJA KICHWA NGUMU





Timu ya soka ya Simba SC leo imeendelea kuusotea ushindi baada ya kubanwa mbavu na wenyeji Majimaji ya Songea kwa suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Majimaji mjini humo.

Mchezo huo ambao ulionekana kutopewa kipaumbele na wachezaji wa timu zote mbili hasa kwa kutocheza kwa kujituma, ulisababisha uonekane kupooza kwa muda mwingi.

Katika hali isiyo ya kawaida, kocha mkuu wa Simba SC, Jackson Mayanja alichukua maamuzi magumu kwa kuwaweka jukwaani wachezaji wote wa kigeni na kuchezesha wazawa pekee.

Kwa mujibu wa karatasi ya orodha ya wachezaji, Mayanja aliwaanzisha wachezaji 11 wazawa huku wale wa akiba pia wakiwa wazawa ambapo pia wachezaji hao wa akiba idadi yao haikutimia kama inavyotakiwa iwe.

Kitendo cha Manyanja kuwaweka benchi wachezaji wa kigeni, kinadhihirisha ukweli wa fununu za hivi karibuni zilizodai kwamba wachezaji hao walipanga kufanya mgomo baridi ikiwemo kucheza chini ya kiwango katika mchezo wa leo wakishinikiza malipo ya mishahara yao.

Imeelezwa kwamba wachezaji hao wanadai malimbikizo ya mishahara yao lakini viongozi amekuwa wakiwazungusha.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment