POLAND YATINGA ROBO FAINALI EURO 2016




 

SAINT ETIENNE, Ufaransa



Mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 imemalizika jioni ya leo huko Ufaransa na kushuhudia Poland ikitinga robo fainali baada ya kuinyuka Uswisi kwa penati 5-4
katika Uwanja wa Geoffroy-Guichard mjini Saint-Etienne, Ufaransa
  .

Kabla ya mchezo huo kuingia hatua ya matuta, timu zote zilikuwa zimetoka sare ya 1-1.

Poland ilitangulia kupata bao kupitia kwa Jakub Blaszczykowski kabla ya Xherdan Shaqiri kuisawazishia Uswisi kwa staili ya tik tak.

Baadae mchezo ulilazimika kwenda kwenye hatua ya penati tano tano na ndipo Poland iliposhinda kwa penati 5-4.

Poland sasa itacheza na mshindi kati ya Croatia na Ureno katika Robo Fainali Alhamisi Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment