YANGA YAREJEA KUTOKA UTURUKI, UONGOZI WATOA MSIMAMO




Na Arone Mpanduka
Msafara wa kwanza wa timu ya Yanga umerejea Dar es Salaam mapema leo(Jumamosi Juni 25) kutoka Antalya, Uturuki, walipokuwa wameweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne.

Yanga watakuwa wenyeji wa mabingwa wa mara tano Afrika, TP Mazembe Jumanne kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa pili wa Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro amesema kundi lingine litawasili muda wowote leo ambapo kesho kikosi kizima kitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mazoezi.

"Tumezungumza na kocha Hans, ametuambia kwamba kambi ya Uturuki ilikuwa nzuri na wachezaji wameifurahia.Tunawaomba mashabiki waje uwanjani kwa wingi siku hiyo ili waone matunda ya kambi hiyo kutoka kwa timu yao,"alisema.

Katika hatua nyingine Yanga imetaja viingilio viwili katika mchezo wake wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Muro amesema viingilio hivyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP.

Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu mjini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo ambao utaanza Saa 10:00 jioni.

Muro pia amesisitiza kwamba mashabiki wa Yanga watajaza uwanja mzima bila kujali maeneo yalitotengwa.

Mara zote imezoeleka kwamba eneo la mashabiki wa Simba hutumiwa na wahusika wenyewe bila kuchanganya na wale wa Yanga.

“Kwa mamlaka niliyopewa na uongozi wa Yanga ni kwamba majukwaa yote yatakaliwa na mashabiki wetu na kama TFF inataka kuchukua adhabu basi iniadhibu mimi kwa niaba ya wengine,” alisema.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment