YANGA YACHECHEMEA


Hali imeendelea kuwa mbaya kwa timu ya soka ya Yanga baada ya hii leo(Julai 16) kuambulia sare katika mchezo wake wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ya nchini Ghana.

Mchezo huo ambao umepigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam jioni ya leo, Yanga imeambulia sare ya bao 1-1 na kuifanya iwe na wakati mgumu katika kundi lake la A hasa ikizingatiwa kwamba tayari ilipoteza mechi mbili za mwanzo.

Donald Ngoma alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya kwanza ya mchezo huo akitumia vema makosa ya safu ya ulinzi ya Medeama na kuiweka timu yake mbele ya Medeama kwa bao 1-0.

Medeama walisawazisha bao hilo dakika ya 17 baada ya Bernard Danso kuunganisha mpira wa kona na kufanya matokeo kuwa 1-1 ambayo yalidumu hadi dakika 90 zinamalizika.

Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya mwisho kwenye kundi lake ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu bila ushindi huku ikiwa imepoteza mechi mbili.

Yanga ilifungwa goli 1-0 ugenini na MO Bejaiya ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A kabla ya kukubali kichapo kingine kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment