MAGUFULI MGENI RASMI MECHI YA TAIFA STARS, STARS KAZI TU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Jumamosi kati ya Taifa Stars na Algeria utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Uswisi mwaka 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mchana wa leo,Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Said Meck Sadik amesema wana uhakika wa asilimia nyingi za kuwepo kwa Rais Magufuli kwenye mchezo huo.
Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu tangu atwae kiti cha Urais.

0 comments:
Post a Comment