Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba
amesema wana makubaliano ya kurejea katika klabu hiyo pindi atakapostaafu
kucheza na anataka kuwa meneja.
Drogba ambaye kwasasa anacheza soka lake nchini
Canada, amewahi kufunga mabao 164 katika vipindi viwili tofauti alivyoichezea
Chelsea.
Akihojiwa Drogba mwenye umri wa miaka 37, amesema
anataka kulipa fadhila kwa klabu hiyo ambayo ilimpa vitu vingi jambo ambalo
amekubaliana na wakurugenzi.
Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa anaweza kurejea
klabu hapo kuchukua nafasi yeyote kama mkufunzi wa shule ya michezo ya timu
hiyo, mshauri wa safu ya ushambuliaji, mkurugenzi wa michezo au hata meneja.
Drogba alifunga penati ya ushindi iliyowapa taji la
Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 na kushinda taji la nne la Ligi Kuu katika
kipindi chake cha pili alichorejea msimu uliopita kabla ya kujiunga na Montreal
Impact inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS.

0 comments:
Post a Comment