Baada ya mechi za jana na juzi za Champions League
kinachofuata ni kuangalia nani ana nafasi ya kusonga mbele na nani yuko
hatarini.
KUNDI A
Real Madrid inasonga mbele kama washindi wa kundi
huku PSG ikisonga pia baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya pili.
KUNDI B
Hadi sasa bado hakuna timu ‘inayosomeka’.Wolfsburg,
Manchester United na PSV Eindhoven bado zinapambana zikiwania hizo nafasi mbili
za juu za kutinga 16 bora.
KUNDI C
Timu za Atletico Madrid na Benfica zimejihakikishia
kutinga 16 bora isipikuwa mechi zao za mwisho zitaamua nani anashika nafasi ya
kwanza na nani anashika ya pili.
KUNDI D
Juventus na Manchester City nazo zote zimetinga 16
bora isipokuwa mechi zao za mwisho zitaamua nani anashika namba moja na nani ya
pili.
KUNDI E
Barcelona katika kundi hili haina mpinzani, imesonga
mbele moja kwa moja baada ya kuongoza kwenye kundi kwa pointi nyingi huku
ikiwaacha Roma, Bayer Leverkusen na BATE Borislov zikigombania nafasi ya pili.
KUNDI F
Katika kundi hili Bayern Munich wamesonga mbele
lakini nafasi ya pili bado inawaniwa na Arsenal na Olympiakos.
KUNDI G
Hapa timu mbili zina uhakika wa kusonga mbele kati
ya Chelsea, Porto na Dynamo Kiev.
KUNDI H
Zenit St Petersburg imesonga mbele kama mshindi wa
kundi na moja kati ya Gent ama Valencia itasonga mbele.

0 comments:
Post a Comment