![]() |
| Baadhi ya wanakamati ya Taifa Stars, Michael Wambura(wa kwanza kushoto), Faroukh(katikati) na Teddy Mapunda (kulia) |
Na Nicolaus Kilowoko
Siku chache baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars kupoteza mchezo wake wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la
Dunia dhidi ya Algeria, hatimaye hii leo Kamati ya kuisaidia timu hiyo yavunjwa
rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo(Nov
26,2015), Mwenyekiti wa kamati hiyo Faroukh Baghoza alisema muda wa kuendelea
na kamati hiyo umekwisha kwa sababu kamati iliundwa kwa lengo la kuhakikisha
timu inafanya vizuri dhidi ya Algeria na kwenda kwenye hatua ya makundi ya
kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia, kitu ambacho hakikuwezekana baada ya
Stars kufungwa mabao 7-0.
Kwa upande wa
Makumu Mwenyekiti wa kamati hiyo Michael Wambura alisema anawashukuru Watanzania
kwa umoja waliouonyesha kwa kuiunga mkono Taifa Stars katika na kuwaomba kuendelea na moyo huo katika
mechi zingine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik
alisema pamoja na kupoteza mchezo huo kwa magoli 7-0 dhidi ya Algeria lakini
kiwango walichokionyesha Stars kilionyesha wazi kuwa kamati hiyo ili saidia vya
kutosha timu hiyo

0 comments:
Post a Comment