Na Arone Mpanduka
Uongozi wa Azam FC umempa mkataba wa muda mfupi golikipa
wa zamani wa timu za Tanzania Prisons, Yanga na
Simba Ivo Mapunda baada ya
kuridhishwa na uwezo wake.
Ivo alikuwa akifanya mazoezi ya kujiweka fiti na
kikosi cha Azam baada ya kutemwa na klabu ya Simba kabla ya kuanza kwa msimu
huu.
Akizungumza na MPANDUKA BLOG, msemaji wa Azam FC Jaffar Iddi amethibitisha taarifa
hiyo ya kusajiliwa kwa Ivo Mapunda kujiunga na Azam kwa mkataba wa muda mfupi.
“Mkataba huu utampa uhuru wa kutoka na kwenda nje ya
nchi endapo atahitajika na timu zingine kwa sababu alikwisha tutaarifu
kuhusiana na uwezekano huo,”alisema Jaffar
Mapunda amekuwa akifanya mazoezi na klabu ya Azam
kwa miezi mitatu sasa tangu alivyoachwa na klabu ya Simba kwa madai kwamba
alikuwa akikwepa kusaini mkataba mpya aliokuwa akipewa na uongozi wa timu hiyo
kitu ambacho Mapunda alisema si kweli.
Ivo Mapunda amewahi kuvitumikia vilabu kadhaa vya
nje ya nchi ikiwemo St George ya Ethiopia pamoja na klabu ya Gor Mahia ya Kenya
kabla ya kurejea nchini na kujiunga na ‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba.

0 comments:
Post a Comment