Klabu ya New York City inayoshiriki Ligi Kuu ya soka
nchini Marekani maarufu kama ‘MLS’ imemteua mchezaji wa zamani wa klabu ya
Arsenal na timu ya Ufaransa Patrick Vieira kuwa kocha mpya wa timu hiyo
kuchukua nafasi ya kocha Jason Kreis.
Kabla ya kujiunga na timu ya New York City ,Vieira
amekuwa kocha wa timu ya vijana na ile ya wachezaji wa akiba ya Manchester City
nafasi ambayo amedumu nayo kwa muda wa miaka 5.
Klabu ya New York City haifanyi vizuri katika Ligi
ya Marekani pamoja na usajili mubwa wa nyota wa soka duniani kama Frank Lampard
mchezaji wa zamani wa vilabu vya West Ham United,Chelsea na Manchester City
pamoja na Andrea Pirlo nyota wa zamani wa klabu za AC Milan na Juventus lakini
bado timu hiyo imeshindwa kufuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Marekani.
Akizungumzia juu ya uteuzi wa Patrick Vieira kama
kocha mpya wa klabu ya New York ,Rais wa klabu ya New York City Tom Glick
anasema kuwa “uteuzi wa Vieira umezingatia vitu vingi vikiwepo nidhamu yake na
mtazamo chanya aliokuwa nao wa kuifanya klabu ya New York City kuwa ya
ushindani katika Ligi ya Marekani hapo baadae.”

0 comments:
Post a Comment