Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano
Ronaldo usiku wa jana amefanya uzinduzi wa filamu yake iitwayo Ronaldo.
Uzinduzi huo umefanyika jijini London, England na
kuhudhuriwa na wageni kadhaa huku kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex
Ferguson akionekana kuwa mgeni aliyevutia zaidi.
Ronaldo alimkaribisha Ferguson kwa bashasha ikiwa ni
pamoja na kumkumbatia.
Naye kocha Jose Mourinho aliyewahi kuwa bosi wa
Ronaldo pale Real Madrid pia alijitokeza.
Wengine waliohudhuria katika uzinduzi huo ni Radamel
Falcao, Carlo Ancelotti, Jorge Mendez, Garry Nevile pamoja na mtangazaji wa
michezo wa kituo cha British Sports TV (Bt Sports) Hayley Mcqueen
Ronaldo aliongozana na mama yake mzazi, maria
Dolores pamoja na mtoto wake, Ronaldo Jr.
Filamu hiyo iliyotengenezwa kwa zaidi ya miezi 14,
imeongozwa na muongozaji muingereza Anthony Wonke ambayo maudhui yake makuu ni
kuonyesha maisha ya nyota huyo tangu alipokuwa mtoto hadi sasa.
![]() |
| Jose Mourinho naye hakuwa nyuma |
![]() |
| Sir Ferguson naye alikuwepo kumsapoti kijana wake |



0 comments:
Post a Comment