Taifa Stars imepoteza mechi yake ya kirafiki ya
mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kwa kufungwa mabao
2-0.
Mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Eldorado nje
kidogo ya jiji la Johanesburg na muda mwingi vijana hao wanaofundishwa na Shau
Bartlet aliyewahi kuchezea Charlton Athletic ya England na Bafana Bafana
walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa kiasi kikubwa.
Baada ya mechi hiyo, Kocha Charles Boniface Mkwasa
alisema wachezaji wake walicheza kwa tahadhari kubwa kwa hofu ya kuumia.
"Lakini kikubwa lilikuwa ni suala la mazoezi na
kuangalia makosa ni nini na kipi cha kurekebisha," alisema Mkwasa.
Baada ya mechi hiyo, Stars imemaliza rasmi kambi
yake ya hapa Afrika Kusini na kesho inaanza safari kurejea nyumbani.
Kikosi
cha Kikosi kilichoanza leo:
1. Aishi
Manula
2. Shomari
Kapombe
3. Haji
Mwinyi
4. Nadir
Haroub
5. Kelvin
Yondani
6. Jonas
Mkude/Himid Mao
7. Simon
Msuva
8. Salum
Abubabary/Frank Domayo
9. John
Bocco/Elius Maguri
10.Mrisho Ngassa/Malimi Busungu
11. Farid Mussa/Salum Telela
CHANZO
CHA HABARI; SALEH JEMBE BLOG
0 comments:
Post a Comment