Timu ya soka ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars imezidi kupata wadhamini baada ya hoteli kubwa ya Serena ya jijini Dar es salaam kutoa sapoti ya chakula na malazi kuelekea katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Algeria.
Stars inarejea leo kutoka nchini Afrika Kusini ilikokuwa imeweka kambi ya siku 10.
Maana yake ni kwamba Stars ikirejea itashusha majeshi yake kwenye hoteli hiyo ya kifahari.
Mdhamini mwingine aliyejitokeza kuongeza nguvu kwa Stars ni benki ya Equity.
Zifuatazo ni picha zingine zinazoonyesha mandhari ya hoteli ya Serena.




0 comments:
Post a Comment