ZIJUE TETESI ZA USAJILI TANZANIA BARA



Kuna tetesi kwamba klabu ya soka ya Azam FC inataka kumsajili kipa Ivo Mapunda ambaye kwa sasa hana timu tangu alipotemwa na Simba SC.Kwa muda mrefu Ivo amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wa Azam FC ili kujiweka fiti.

Kuna tetesi kwamba klabu ya Simba inasikilizia kumalizika kwa michuano ya Chalenji ili iweze kufanya mazungumzo ya kina na mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Paul Kiongera.

Pia klabu hiyo ina mpango wa kusajili wachezaji wengine wawili zaidi ili kuimarisha kikosi chake.

Tetesi zingine zinadai kwamba Klabu za Toto Africans, Stand United na Mbeya City zinamfukuzia mshambuliaji wa Yanga Simon Matheo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment