BONDIA MASHALI AJIFICHA 'KICHAKANI'

Na Arone Mpanduka

Bondia Thomas Mashali amejificha mahali kusikojulikana akijiandaa na pambano la kumaliza ubishi dhidi ya Francis Cheka

Pambano hilo limepangwa kufanyika katika Sikukuu ya Krismass ya Disemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Akizungumza na MPANDUKA BLOG kwa njia ya simu, Mashali alisema mazoezi yake yanaendelea vema isipokuwa hataki watu wajue mahali anapofanyia maandalizi hayo.

"Mashabiki wangu nawaambia tukutane Jamhuri lakini wasitake kujua nilipo kwa sasa"

Kwa upande wake Cheka, anafanya maandalizi yake huko mjini Morogoro ambako ndiko makazi yake yalipo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment