![]() |
Na Arone Mpanduka
Timu ya soka ya Mbeya City imeanza kuipiga mkwara Yanga kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na MPANDUKA BLOG kwa njia ya simu,kocha mkuu wa Mbeya City Meja mstaafu Abdul Mingange alisema timu yake ipo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Alisema maandalizi waliyofanya ni kwa ajili ya Ligi nzima na si Yanga pekee.
"Sisi muda wote tupo tayari kama askari vile na Jumamosi tutachukua pointi tatu"
"Tunatambua kuwa Yanga imeanza vizuri msimu lakini na sisi ni timu nzuri pia"
Mingange alisema kwa sasa wamejificha na wataonekana siku yenyewe ya mechi.

0 comments:
Post a Comment