Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del
Bosque amepanga kustaafu baada ya kumalizika kwa fainali za Euro
zitakazofanyika nchini Ufaransa mwaka 2016
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid mwenye umri wa
miaka 64 aliiongoza Hispania kutwaa ubingwa katika fainali za dunia za mwaka
2010 na Euro 2012.
Amesema muda wake wa kustaafu unakaribia na kwamba
endapo kila kitu kitakwenda vizuri atastaafu baada ya fainali za mwaka 2016.

0 comments:
Post a Comment