Bosi wa klabu ya soka ya Chelsea Roman Abramovich
ana matumaini makubwa ya kumleta Pep Guardiola Stamford Bridge baada ya
kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Jose Mourinho, kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail.
Kocha huyo anayeinoa miamba ya soka nchini Ujerumani
klabu ya Buyern Munich mkataba wake unaisha mwakani na anaweza akatangazwa kuwa kocha wa Chelsea klabla
ya mkataba wake haujaisha.
Kuna taarifa kuwa klabu ya Mancherster City
inamyemelea kocha huyo kuchukua mikoba
ya Manuel Pellegrini lakini Abramovich aliyemtimua Jose Mourinho Alhamis iliyopita anahitaji kumchukua kocha
ndani ya klabu yake.
Bilionea huyo wa Urusi anajipanga kutumia fedha
nyingi kwa ajili ya kuhakikisha kocha huyo mwenye miaka 44 anatua darajani.

0 comments:
Post a Comment