MAJABVI AIPIGIA MAGOTI SIMBA SC

Baada ya malumbano ya muda mfupi kati yake na uongozi wa klabu ya Simba hatimaye Mzimbabwe Justice Majabvi amekubali yaishe na kuomba arejeshwe kikosini.

IFUATAYO NI TAARIFA RASMI YA UONGOZI WA SIMBA SC

Simba sports club
Dar es salaam
23-12-2015

Taarifa kwa vyombo vya habari

Klabu ya Simba inapenda kuufahamisha umma kuwa mchezaji wake toka Zimbabwe Justice Majabvi ameomba kurejea kwenye timu baada ya kutafakari upya uamuzi wake wa awali wa kutofanya mazoezi na wenzake.
Leo mchezaji huyo amejiunga na wenzake waliopo kanda ya ziwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya klabu ya Mwadui ya Shinyanga jumamosi hii.

Hata hivyo klabu ya Simba pamoja na kumpokea na kumruhusu mchezaji huyo kwenda huko. Imelipeleka suala la mchezaji Justice Majabvi katika kamati ya nidhamu ya klabu ili kuona hatua za kuchukua kama kutakuwa na ukiukwaji wa maadili ya kinidhamu ikiwa ni pamoja na Majabvi kutofanya mazoezi na timu kwa zaid ya siku tano, kutoambatana na timu kanda ya ziwa na kuongea na vyombo vya habari bila ya ruhusa maalum ya uongozi kinyume na mkataba wake na Klabu.

Tunaamini jambo hili litamalizika kwa njia sahihi na kwa kuzingatia maslah ya pande zote mbili klabu na mchezaji mwenyewe.

Imetolewa na Haji S Manara
Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba

Simba nguvu moja
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment