Katibu Mkuu wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar
Kassim Haji Salum amesema timu za Gor Mahia ya Kenya , KCCA ya Uganda , Yanga,
Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Tanzania Bara na Mafunzo na JKU kutoka
visiwani Zanzibar ndio zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Januari 2 mwakani
visiwani humo.
Amesema michuano ya Mapinduzi Cup itazisaidia timu
za Yanga, Azam FC, JKU na Mafunzo kujiandaa na Mashindano ya CAF ya vilabu
Barani Afrika.
Yanga watacheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa mchezo
wa mtoano na timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius wakati Azam FC watacheza na
mshindi kati ya klabu ya Seychelles na Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika
Kombe la Shirikisho.
Mafunzo ya Zanzibar, wao watacheza na klabu ya AS
Vita ya Congo DR kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika na timu ya JKU
itashiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Gaborone United ya Botswana.
Hadi sasa Simba ndiyo mtetezi wa kombe hilo baada ya
kushinda Januari mwaka huu kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment