Na Arone Mpanduka
Timu ya soka ya Yanga imeamua kuachana na mchezaji
wake Mbrazil Andrew Countinho ili iweze kuongeza kifaa kingine kutoka nchini Niger
Issouf Bubakar Garba, imefahamika.
Taarifa ambazo MPANDUKA BLOG imezinasa kutoka kwa
mtu wa karibu wa timu hiyo, Countinho ameonekana kutowaridhisha viongozi wa
Yanga hasa kufuatia kushuka kwa kiwango chake.
Kufuatia hali hiyo, Mbrazil huo ‘anakuwa mbuzi wa
kafara’na kwa sababu pengo la mchezaji mmoja litakuwepo, Yanga watalazimika
kulitumia vema dirisha la sasa la usajili kwa kumleta Mniger huyo.
Hata hivyo MPANDUKA BLOG iliamua kwenda mbali zaidi
na kuwatafuta wahusika ambapo Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa
Yanga, Jerry Muro alionekana kujibu kwa kusitasita, jambo ambalo limeonyesha
kuwa na ukweli isipokuwa klabu haijajiandaa kutoa taarufa rasmi kwa sasa.
“Huenda taarifa hizo zikawa hazina ukweli ama kwa upande
mwingine pia zikawa kweli lakini niwahakikishie wana Yanga kwamba siku ya
Ijumaa tutafanya mkutano na waandishi wa habari na kuwaeleza kila kitu”

0 comments:
Post a Comment