Beki wa zamani wa Arsenal, Kolo Toure amesema Uwanja
wa Emirates ndio chanzo kikubwa cha klabu hiyo kushindwa kunyakuwa taji la Ligi
Kuu katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Arsenal walikuwa wakitumia Uwanja wa Highbury kabla
ya kuamua kujenga uwanja mpya wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ambao
walihamia mwaka 2006.
Taji la mwisho la ligi kuchukuliwa na Arsenal
ilikuwa msimu wa 2003-2004 wakati klabu hiyo ilipomaliza msimu bila kufungwa na
wamenyakuwa mataji manne pekee toka wakati huo.
Lakini Toure amempongeza meneja wa timu hiyo Wenger
kwa juhudi zake toka wakati huo baada ya klabu kulazimika kupunguza matumizi
kwa miaka kadhaa ili kuweka mahesabu yao sawasawa.
Toure amesema ingawa hayuko katika klabu hiyo lakini
kuna mambo mengi yalibadilika, wachezaji wengi waliondoka akiwemo Patrick
Vieira hivyo iliwawia vigumu lakini sera hiyo ilianza wakati wameanza ujenzi wa
uwanja mpya.
Toure aliendelea kudai kuwa Arsenal ililazimika
kuuza nyota wake akiwemo Robert Pires, Thiarry Henry na kulazimika kuanza
kutegemea wachezaji chipukizi wasiokuwa na uzoefu wowote.

0 comments:
Post a Comment