Vyombo vya habari nchini Ureno, vimeripoti kuwa
sanamu la Cristiano Ronaldo lililopo huko Fanchal, mji mkuu wa kisiwa cha
Madeira liliamiwa na wahuni na kupakwa rangi ya jina na namba anayovaa Lionel
Messi.
Tukio linadaiwa kufanyika usiku wa kuamkia Jumanne,
saa chache baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Agentina na Barcelona kutwaa
tuzo yake ya tano ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia maarufu kama Ballon d’Or
akimshinda Ronaldo.
Jina la Messi pamoja namba 10 zote zilichorwa kwa
rangi nyekundu katika sanamu hilo kabla ya wahusika kwenda kusafisha sanamu
hilo na kufuta kilichoandikwa.
Akihojiwa dada yake Ronaldo, Katia Aveiro amesema
tukio hilo ni la aibuna linaonyesha jinsi wanamuonea wivu ndugu yake huyo.
Ronaldo alizindua sanamu hilo la shaba lenye urefu
wa mita 3.40 Desemba mwaka 2014, mita chache kutoka katika makumbusho yake
mwenyewe aliyotengeneza katika mji huo.

0 comments:
Post a Comment