MAKALA: SAA YA MAYWEATHER KUMLIPA OBAMA MIAKA MIWILI



HIVI karibuni bondia mstaafu Floyd Mayweather alinunua saa ya mkononi kwa gharama ya dola milioni 1.1 ambayo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya bilioni mbili.

Saa hiyo aina ya Hublot inaelezwa kwamba ndiyo ghali zaidi duniani kwa sasa.
Mayweather alinunua saa hiyo akiwa nchini Dubai ambako alikwenda kama sehemu ya matembezi yake katika nchi mbalimbali za kifahari duniani.

Ikumbukwe kuwa Mayweather alipita nchini Uturuki na pia alikwenda nchini Ufaransa katika matembezi hayo binafsi huku akitumia chopa yake  ya bei ghali.

Saa hiyo ya Hublot ambayo bondia huyo anaimiliki kwa sasa imetiwa nakshi mbalimbali huku ndani yake kukiwa na kiasi kidogo cha almasi.

Mayweather ambaye anatoka katika taifa la Marekani kwa maana kwamba ni raia wa nchi ya Marekani, amenunua saa ambayo thamani yake inazidi kiwango cha mshahara anacholipwa rais wa Marekani Barack Obama kwa mwaka.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa mtandao wa Africa Review uliotolewa mwezi Julai mwaka jana, Obama anapokea mshahara wa kiasi cha dola 400,000 kwa mwaka.

Kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba saa ya Mayweather inaweza kumlipa Obama mshahara wa miaka miwili huku kiasi kingine cha pesa kikibaki.
Hiyo ni kufuru ya aina yake kwa bondia huyo mstaafu ambaye amekuwa akitumia pesa kwa fujo bila ya kujali anachokipoteza.

Kwa namna moja ama nyingine pia inaweza kuwa kejeli kwa Obama ambaye ni Rais wa taifa lake, na si taifa hilo pekee, kwani ni Rais mwenye nguvu duniani na kufanya watu wamuite mbabe wa dunia.

Kwa nchi zilizoendelea, Obama ndiye anayeongoza kwa kulipwa kiasi kikubwa cha mshahara akifuatiwa na Stephern Harper wa Canada anayekunja kiasi cha dola 260, 000 kwa mwaka huku Kansela wa Ujerumani, Angela Markel akiwa anakunja kiasi cha dola 234,000 kwa mwaka.

Tukirejea kwenye saa ya Mayweather, kama akiamua kumlipa Harper basi anaweza kumlipa mshahara kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Hiyo  ni kwa sababu ukichukua dola milioni 1.1 na kutoa dola 260,000 utagundua kwamba kiasi kitakachobakia ni kingi mno.

Kwa upande wa Angela Markel, gharama ya saa ya Mayweather inaweza kumlipa mshahara kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo, tena bila wasiwasi wowote.

Mbali na hilo Mayweather kwa kutumia gharama ya saa yake anaweza kuwalipa mshahara wa mwaka mmoja vigogo hao watatu kwa mara moja.

Hiyo ni kwa sababu ukijumlisha mshahara wa Obama, Harper na Markel unapata jumla ya dola 894,000 ambazo si jambo gumu kuwalipa wote watatu.

KUFURU ZINGINE ZA MAYWEATHER
Mwezi Januari mwaka huu Mayweather alipiga picha akiwa mbele ya ndege yake  binafsi na magari manane ya thamani kubwa anayoyamiliki.

Mayweather, anayetajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya pauni milioni 66.1, imeelezwa kuwa thamani ya magari yote manane anayoyamiliki ni pauni milioni tano.

Mali zote hizo aliamua kuzipiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Pia aliwahi kutumia pauni 17,000 (zaidi ya milioni 40 za kitanzania) kwa ajili ya vifaa vya kukinga kinywa (gum shield) katika pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao lililofanyika kwenye ukumbi wa Las Vegas, Marekani Mei 2 mwaka huu.

Aliamua kutumia gharama kubwa kutengeneza vifaa hivyo kwa kutumia dhahabu, vumbi la almasi na vipande vya fedha halisi, vyote vikichanganywa katika plastiki na kuandikwa jina lake. 

Bondia huyo alisema amelazimika kutengeneza vifaa hivyo vya kifahari kwa madai kwamba vitalinda meno yake na kumsaidia kupumua vizuri wakati wa pambano.

mpanduka@yahoo.com
0786 160643
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment