Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen huenda akarejea kwenye julumu lake la kuzinoa timu za taifa za vijana.
Mei 11 mwaka 2012 kocha huyo alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu ww Taifa Stars baada ya kutimuliwa kwa Jan Poulsen
Kabla ya kupewa Taifa Stars kipindi hicho Kim alikuwa anafundisha timu za taifa za vijana.
Hata hivyo jahazi la Taifa Stars lilimshinda raia huyo wa Denmark na ndipo mwishoni mwa mwaka 2013,Shirikisho la soka nchini TFF chini ya Rais Jamal Malinzi likavunja mkataba wake na kumleta Mart Nooij mwaka 2014.
Lakini jana rais wa TFF Jamal Malinzi aliweka picha kwenye ukurasa wake wa twitter ikimuonyesha akiwa anapata chakula cha mchana na kocha huyo, jambo ambalo limezua mijadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba huenda wanafanya mazungumzo ya kutaka kumrejesha tena kwenye timu za vijana.
Timu za taifa za vijana zimekuwa hazina kocha maalum tangu kuondolewa kwa Kim Poulsen ambaye alionekana kufanya vizuri akiwa na timu hizo.
Mfano mzuri ni timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 mbayo kocha Adolf Rishard aliwahi kuteuliwa kufundisha kabla ya kuomba kujiuzulu na sasa timu hiyo ipo chini ya kocha Sebastian Mkomwa.

0 comments:
Post a Comment