BARCELONA YATINGA FAINALI COPA DEL REY

Barcelona wamefika fainali ya Copa del Rey baada ya kutoka sare na klabu ya Gary Neville Valencia na kukamilisha ushindi wa jumla wa 8-1.

Barca walitoka sare 1-1 na Valencia kwenye mechi ya marudiano katika uwanja wa Mestalla usiku wa jana Jumatano.

 Mechi ya kwanza walikuwa wamepata ushindi wa 7-0 uwanjani Nou Camp, ushindi uliowafanya wengi kutoa wito kwa Neville, nyota wa zamani wa Manchester United, kujiuzulu.

Valencia ndio waliotangulia kufunga mechi hiyo ya Jumatano kupitia Alvaro Negredo.

Lakini nguvu mpya wa Barca Wilfrid Kaptoum alisawazisha dakika za mwisho na kumnyima Neville ushindi.

Matokeo hayo yana maana kwamba Barcelona sasa hawajashindwa katika mechi 29, ambayo ni rekodi Uhispania.

Valencia wabebeshwa magoli saba Barcelona
Wapinzani wao kwenye fainali watakuwa mshindi kati ya Celta Vigo na Sevilla.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment