Shabiki mmoja wa klabu ya Leicester City huenda
akajishindia pauni 25,000 iwapo timu hiyo itashinda taji la Ligi kuu ya
Uingereza baada ya kuweka pauni tano katika dau la paundi 5,000.
Ushindi wa Leicester wa mabao 3-1 dhidi ya
Manchester City unawaacha wakiwa mbele kwa pointi tano katika msimamo wa Ligi
huku Ligi hiyo ikiwa imefikia kwenye robo tatu ya mechi zake.
Carpenter Leigh Herbert, mwenye umri wa miaka 38 alijaribu
bahati hiyo akiwa katika likizo na amekataa ombi la kumtaka achukue pauni 3,200
ili kujiondoa.
Iwapo Leicester ambao walikuwa chini ya msomamo wa
ligi hiyo mwaka mmoja uliopita watashinda taji hilo la ligi,inaaminika kuwa
hiyo itakuwa zawadi kubwa kuwahi kutolewa katika historia ya michezo.

0 comments:
Post a Comment