NJAA YAENDELEA KUITAFUNA COASTAL UNION



Unayoiona hapo juu ni taarifa(post) aliyoisambaza mchezaji wa Coastal Union Sabo Youssoufa akishinikiza malipo ya mshahara.

Beki huyo mwenye uraia wa Cameroon ameanika taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii akiutaka uongozi wa klabu hiyo ya Tanga kumrejeshea pasi yake ya kusafiria haraka pamoja na pesa zake za usajili na malimbikizo ya mishahara.

Coastal Union bado inaandamwa na jinamizi la ukata ambapo inasemekana hadi sasa wachezaji wake wanadai mishahara yao.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment