Yanga SC Jumamosi ya leo imesonga mbele kwenye
michuano ya klabu bingwa Afrika licha ya kutoka sare ya 1-1 APR ya Rwanda kwenye
mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
APR ambao
walipoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 jijini Kigali, waliwashtua Yanga mapema
katika dakika ya tatu baada ya winga Fiston Nkinzingabo kuifungia timu yake bao zuri akimalizia krosi
ya Rusheshangonga Michel.
Bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 28 ya
mchezo, Donald Ngoma alisawazisha na kufanya sare hiyo idumu kwa kipindi chote
cha dakika 90.
Yanga imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya
mchezo wa awali kushinda ugenini 2-1.
Baada ya mchezo kumalizika Mkuu wa Kitengo cha
Habari na Mawasiliano wa Yanga , Jerry
Murro alikiri kamba mchezo ulikuwa mgumu na kuongeza kwamba sasa
wanageukia viporo vyao vya Ligi Kuu Tanzania Bara.

0 comments:
Post a Comment