SERENA WILLIAMS ALA CHAKULA CHA MBWA

Nyota wa mchezo wa tenisi kwa upande wa wanawake Serena Williams alijitia ugonjwa baada ya kula chakula cha mbwa saa chache kabla ya kufuzu katika robo fainali ya mashindano ya Italian Open.

Serena alijaribu kula kijiko kimoja cha chakula cha mbwa wake kabla ya kumshinda Mmarekani mwenzake Christina McHale katika seti za moja kwa moja.

''Nilisema kwani kuna nini,nitajaribu kipande kimoja,kinaonja utamu'',alisema.

''Lakini mda mchache nililazimika kukimbia chooni kama ambaye ningezimia''.

''Chakula kilikuwa na ladha mbaya''.
''Kinaonja kama dawa ya kusafisha nyumba''.

Katika video ya Snap chat ,wiliams alielezea kuwa alichukua samaki na wali uliokuwa katika chakula kilichopewa mbwa katika hoteli aliyokuwa akilala.

''Nilijilazimisha kula'',alisema mchezaji huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 34.

''Sijui wanatia nini katika chakula hiki cha mbwa,lakini mbwa alikipenda sana''.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment