MTIBWA YAIBUTUA STAND ASUBUHI YA LEO

Mtibwa leo imefanikiwa kulinda ushindi wake wa bao 1-0 iliyoupata jana katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Stand United.

Mchezo huo umepigwa leo asubuhi ikiwa ni muendelezo wa mechi iliyovunjika jana kwenye uwanja wa Manungu kufuatia mvua kubwa liyonyesha.

Mechi hiyo ya jana ilivunjika katika dakika ya 45 huku Mtibwa ikiongoza bao moja.

Dakika 45 zingine za mechi hiyo zimechezwa leo baada ya jana kuchezwa kipindi kimoja na mechi kuahirishwa kutokana na mvua kubwa.

Bao la jana lilifungwa na Muzamiru Yassin akiunganisha mpira wa kona wa Shiza Kichuya.

Kwa ushindi huo wa leo,.Mtibwa imejiongezea pointi na kufikisha 31 huku bado ikiwa nafasi ya nne.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment