HAJI MANARA KWENDA INDIA KESHO KWA MATIBABU

Na Nicolaus Kilowoko

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano cha klabu ya Simba, Haji Manara kesho anatarajiwa kukwea pipa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya macho.

Manara alipatwa na matatizo hayo hivi karibuni ambapo jicho lake moja lilipoteza uwezo wa kuona na lingine likiwa linaona kwa kiasi kidogo.

“Ninapenda niliweke sawa hili, Mimi sikuomba watu wanichangie pesa za matibabu isipokuwa walioguswa na tatizo langu ndiyo waliojitokeza na kunichangia.Ninawashukuru walionichangia. Manake nimeona niwaeleweshe watu ili isije ikaonekana kwamba Haji anaomba msaada,”alisema Manara.

Siku chache zilizopita baadhi ya wanachama wa Yanga wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Jerry Muro, walikwenda nyumbani kwake na kumkabidhi kiasi cha shilingi 1,055,000 ambacho walichangishana kupitia makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii.

 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment