Timu ya soka ya Simba leo imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika mwaka 2016 baada ya kuinyuka Ndanda FC ya Mtwara bao 1-0.
Bao pekee la Simba limefungwa na kinda Ibrahim Hajib katika mchezo ambao umechezwa jioni kwenye dimba la Nangwanda Sijaona huko Mtwara.
Huenda ushindi huo ukaashiria mambo mazuri kwa Simba katika mwaka wote wa 2016.
Mechi hiyo ya ligi kuu ni ya kwanza katika mwaka huu wa 2016.
Baada ya mchezo huo, Simba itakwenda Zanzibar kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya Mapinduzi.
Simba itakwenda kutetea taji hilo ikiwa bingwa mtetezi baada ya Januari 13 mwaka jana kutwaa kombe kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar.
0 comments:
Post a Comment