MATOLA AOTA MBAWA SIMBA

Matola



















KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amejiuzulu rasmi nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutoelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo, msemaji mkuu wa klabu ya soka ya Simba Hajji Manara amesema Matola ameongea na Rais wa klabu ya soka ya Simba na kumwambia hataki kuendelea kuwepo kwenye banchi la ufundi kutokana na ugomvi wake na kocha mkuu wa klabu hiyo Kerr.

Manara amesema uongozi wa Simba utajaribu kukaa na kujadili cha kufanya baada ya maamuzi ya Matola.
Dylan Kerr

Historia ya Matola ndani ya Simba SC inaanzia mwaka 2000 alipojiunga nayo kama mchezaji akitokea Kagera Stars (sasa Kagera Sugar) na aliichezea timu hiyo hadi mwaka 2005 alipohamia Super Sport United ya Afrika Kusini.

Lakini baadae alirejea tena kwa wekundu hao kama kocha wa kikosi cha vijana na hapo ndipo uongozi wa Simba ulipoona anafaa kuwa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment