MICHAEL MALUWE KATIBU TBF,ZONGA APIGWA CHINI

Na Arone Mpanduka

Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini imemteua Michael Maluwe kuwa Katibu mkuu ambaye atasaidiwa na Mwenze Kabinda.

Awali nafasi ya Katibu mkuu ilikuwa inashikiliwa na Saleh Zonga ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuhomola zaidi ya shilingi milioni 30 za Shirikisho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Ufundi na Mipango wa TBF, Manase Zablon, kikao hicho kilichoketi Jumamosi kitapeleka majina ya walioteuliwa kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kuthibitishwa na wajumbe.

Katika kipindi cha siku chache zilizopita, Zonga alisimamishwa kwa madai hayo huku akiwa anasubiri maamuzi ya Bodi ya TBF.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment