Timu za Yanga na Azam zimeshindwa kutambiana usiku huu(Jumanne Jan 5)baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Azam FC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 56 baada ya mabeki wa Yanga kujipanga vibaya na mfungaji akavunja mtego na kuuwahi mpira kabla ya kupiga shuti kali lililomzidi Deo Munishi ‘Dida’.
Yanga nao waliendelea kupambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 82 kupitia kwa Donaldo Ngoma baada ya makosa ya kipa Aishi Manula ambaye alidaka mpira na kuudondosha.
Bao la Yanga lilipatikana dakika chache baada ya nahodha wa Azam FC, John Bocco kulambwa kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekundu.
Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe tangu Yanga ilipokuwa nyuma kwa bao moja kwasababu wachezaji wake walionekana kuingiwa na jazba.
Mechi hiyo ilitanguliwa na ya Mtibwa na Mafunzo ambapo Mtibwa ilishinda bao 1-0.

0 comments:
Post a Comment