WACHEZAJI COASTAL UNION WADAI MISHAHARA MIEZI MITATU

Wachezaji wa klabu ya Coastal Union Tanga wameanzisha mgomo baridi wakishinikiza kulipwa mishahara ya miezi mitatu.

Taarifa za uhakika ambazo MPANDUKA BLOG imezinasa zinadai kwamba wachezaji hao hawajalipwa mishahara tangu Novemba mwaka jana, hali iliyochangia mwenendo wao kuwa mbovu katika Ligi Kuu.

Coastal Union kwa sasa inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Inaelezwa kuwa shinikizo hilo limeilazimu timu hiyo kutembea kwa mguu kutoka mazoezini hadi makao makuu ya Klabu na kudai malipo yao leo hii.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment