TIKITI ZA TAMASHA LA TUMAINI JIPYA ZASOGEZWA MTAANI KWAKO

Tikiti za kushuhudia tamasha la Tumaini Jipya lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Redio na TV Tumaini sasa zimesambaa kona zote za jiji la Dar es salaam.

Tamasha hilo la nyimbo za injili litafanyika Julai 31 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo kwaya na waimbaji mbalimbali watashiriki kutoa burudani.

Lengo la tamasha ni kuhamasisha watoto na vijana wa ngazi mbalimbali kuwa na maadili mema kwa maendeleo ya taifa, kwani bila maadili hakuna maendeleo.

Mbali na kusambazwa kwenye Parokia zote za Jimbo Kuu la Dar es salaam, tikiti sasa zimesogezwa mtaani kwako kupitia mawakala mbalimbali kama inavyoonekana orodha yao hapo chini.

Pia hata ukiwa umepumzika nyumbani kwako unaweza kununua tiketi hizo kwa njia ya simu yako ya kiganjani.


Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment