Presha imezidi kupanda kwa kocha David Moyes wa
klabu ya Real Socieded inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania (La Liga) mara
baada ya jana usiku kupokea kichapo cha magoli 2-0 toka kwa Las Palmas ya
nchini humo.
Kipigo hicho ni cha 6 katika michezo 11 iliyochezwa
msimu huu na kuiweka timu hiyo katika mstari wa hatari ya kushuka daraja kwa
tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
David Moyes hivi sasa, anakabiriwa na michezo migumu
dhidi ya bingwa wa UEFA Europa ligi Sevilla na baadaye Barcelona ambao ni mabingwa
wa klabu bingwa barani Ulaya.
Kocha huyo aliyefukuzwa na Manchester United kabla
ya kuingia mkataba na Real Socieded, amebakiza hadi mwisho wa msimu huu
kumalizia mkataba wake aliosaini msimu uliopita kipindi kama hiki.
0 comments:
Post a Comment