Pazia la michuano ya vilabu bingwa Afrika litafungwa
rasmi Jumapili November 8, 2015 pale TP Mazembe watakapo wakaribisha USM Alger
kwenye mchezo wa fainali ya pili jijini Lubumbashi.
Mchezo wa awali ulimalizika kwa Mazembe kupata
ushindi wa bao 2-1 na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa huo
kwa mara ya tano kwenye historia ya klabu hiyo.
USM Alger wanacheza mchezo wa fainali ya vilabu
bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza huku wakiwa bado wanamatumaini ya
kunyanyua ndoo hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu yao.
TP Mazembe tayari imetwaa ubingwa wa vilabu barani
Afrika mara tano.
Wametwaa ubingwa huo mwaka 1967, 1768, 2009 na mara
ya mwisho kutwaa ubingwa huo ilikuwa ni mwaka 2010.
Jumla ya magoli 6 yamefungwa na mshambuliaji wa El
Merreikh ‘El Medina’ Babeker, ambayo ni sawa na ya nyota wa TP Mazembe Mbwana
Samatta.
0 comments:
Post a Comment