Steven Gerrard(kushoto) na Frank Lampard(kulia) wakiwa katika moja ya mazoezi ya timu ya soka ya taifa ya England |
NEW YORK, Marekani
Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Frank
Lampard amekiri kujutia maisha yake katika soka la kimataifa kwa kushindwa kutengeneza ushirikiano mzuri katika safu ya
kiungo na Steven Gerrard.
Viungo hao ambao kwasasa wanacheza soka nchini
Marekani katika klabu za New York City FC na Los Angeles Galaxy, walikuwa nyota
wa kutumainiwa katika klabu zao za Chelsea na Liverpool lakini walishindwa
kabisa kuelewana pindi wanapokutana katika majukumu ya kimataifa.
Makocha waliofundisha kikosi cha timu ya taifa ya
Uingereza walishindwa kuwaunganisha wawili hao wakati wanapokuwa pamoja.
Akihojiwa Lampard amesema anadhani kuna muda makocha
waliokuwa wakiwaongoza walitakiwa kufanya kitu tofauti ili aweze kuelewana
vyema na Gerrard pindi wanapokuwa uwanjani pamoja.
0 comments:
Post a Comment