Kikosi cha Coastal Union |
Na Oscar Assenga, Tanga
Uongozi wa Klabu ya Coastal Union ya
Tanga umewaomba radhi wadau wa soka pamoja na shirikisho la soka nchini TFF kwa
vurugu zilizotokea kwenye mchezo wao dhidi Mbeya City uliofanyika mwishoni mwa
wiki hii katika uwanja wa uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mchezo huo wa ligi kuu soka Tanzania
bara ulimalizika kwa vurugu hadi kikosi
cha kutuliza ghasia (FFU) kilipoingilia kati na kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya mashabiki wa soka waliokuwepo katika uwanja wa Mkwakwani.
Vurugu hizo zilitokea kufuatia mwamuzi
wa mchezo huo Erick Enock kutoka Arusha kuamuru ipigwe penati kuelekea lango la
Coastala union katika dakika za majeruhi na kuiwezesha Mbeya City kusawazisha
bao hivyo hadi matokeo kuwa sare ya fungana bao 1-1.
Coastal Union iliomba radhi katika barua
yake iliyoandikwa na kutiwa saini na Mwenyekiti wake Dr Ahmed Twaha kwenda kwa
Katibu mkuu wa TFF, na nakala nyingine kwa Rais Jamal Malinzi,afisa mtendaji
mkuu bodi ya ligi na katibu wa Chama cha soka mkoa wa Tanga (TRFA).
Aidha baada ya kutokea tukio hilo
Mwenyekiti huyo alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji
kujadili nini cha kufanya na hatua za kuchukua kwa wale watakaobainika kuhusika
kwenye vurugu hizo.
Katika kikao hicho kamati ya
utendaji imelaani vurugu hizo na imeaziamia kuwachukulia hatua waliohusika.
Imetolewa na Ahmed Twaha,Mwenyekiti wa
Coastal Union
0 comments:
Post a Comment