Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameonyesha
dalili kwamba yu tayari kucheza mchezo wa mahasimu kati ya Barcelona na Real
Madrid utakaopigwa Jumamosi hii baada ya kuonyesha rasmi viatu vyake vipya.
Nyota huyo ameonyesha viatu maalum vilivyotengenezwa
na kampuni ya Adidas kwa ajili ya mchezo wa ‘EL Classico’ siku ya Jumamosi.
Viatu hivyo
vimepambwa na rangi nyeusi,kijani na nyekundu.
Messi hajacheza
mchezo wowote tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya Las Palmas mnamo mwezi wa
tisa mwaka huu jambo ambalo linawapa wasiwasi Barcelona kwamba huenda akaukosa
mchezo wa Jumamosi.
Messi
alionekana juzi katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Barcelona akifanya
mazoezi na taarifa za kitabibu toka klabu ya Barcelona zinasema kuwa nyota huyo
anaweza kucheza mechi hiyo ingawa ni mapema kuwa na uhakika wa asilimia 100.
0 comments:
Post a Comment