Mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool amesema
yuko fiti na sasa anataraji kurudi uwanjani mara baada ya kuwa ameanza mazoezi
na kikosi cha kwanza na wachezaji wenzie wa Liverpool.
Sturridge ambaye hajakuwa sawa kwa kipindi cha
takribani miezi 18 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, amerudi tena upya na
anahitaji kutoumia na kufanya kazi ili kujiweka sawa kwa kocha mpya mjerumani
Jurgen Klopp.
Akizungumza katika hafla za uzinduzi wa mavazi ya
klabu akiwa kama mgeni mualikwa, Sturridge amesifia matunda ya kocha mpya
Jurgen Klopp klabuni hapo huku akisema anaona ni wakati mahsusi kwake na kwa
klabu.
Liverpool hivi sasa imekuwa ikimtumia mshambuliaji
raia wa Ubelgiji Christian Benteke pekee.
0 comments:
Post a Comment