RIBERY AISHITAKI CNN
Winga wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya FC Bayern Munich Frank Ribery amekishtaki kituo cha televisheni cha Marekani CNN akikidai fidia ya dola milioni 1.5 sawa na shilingi bilioni 3.2 za Tanzania.
Ribery amefungua kesi hiyo baada ya kituo hicho cha TV kutumia picha ya mwanasoka huyo katika kuelezea story juu ya matibabu ya cryotherapy – matibabu yanayohusisha kuuweka mwili kwenye sehemu kavu au yenye baridi kali ili kupunguza maumivu au kuponyesha kabisa.
“Mr Franck RibĂ©ry … hakutoa ruhusa ya matumizi ya picha ile kwa kituo cha CNN,” alisema Carlo Alberto Busa ambaye ni mwanasheria wa Ribery wakati akiongea na radio ya Ufaransa – RMC
Picha hiyo ya Ribery ilionekana kwenye akaunti ya Twitter ya CNN na Ribery alionekana kwenye box la cryotherapy huku picha ikisindikizwa na kichwa cha habari kifuatacho: “Mwanamke hakutwa ameganda kwenye box la cryotherapy, matibabu haya yazua maswali.”
0 comments:
Post a Comment