Na Arone Mpanduka
Timu ya taifa ya soka la wanawake, Twiga Stars
imetakata jioni ya leo baada ya kuifunga Malawi mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Mabao hayo mawili yamefungwa na Asha Rashid
Mwalala(dakika ya 43) na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’(dakika ya 82).
Lengo kuu la mchezo huo lilikuwa ni kumfanya kocha
Rogasian Kaijage kukitathmini kiwango cha kikosi chake na kujua maendeleo yake
licha ya kutokuwa na mashindano yoyote mbele yake.
‘LUNYAMILA’
ASTAAFU RASMI
Dakika 28 hii leo zilitosha kuhitimisha soka la
kimataifa la winga wa kushoto Esther Chaburuma maarufu kama Lunyamila aliyecheza
kwa muda huo na kisha kwenda kupumzika nje ya uwanja.
‘Lunyamila’ alitumia mchezo huo pia kustaafu rasmi
na kuwaaga wachezaji wenzake wa Twiga Stars.
Ni mchezaji aliyeitumikia timu hiyo kwa kipindi
kirefu tangu mwaka 2002 ambapo nyota yake ilianza kung’ara.
Jina la Lunyamila alilipata katika miaka hiyo
akifananishwa na aliyekuwa winga wa Yanga kwa wakati huo,Edibily Jonas Lunyamila.
0 comments:
Post a Comment