Wagombea watano wa tuzo ya BBC kwa
mwanasoka bora wa mwaka 2015 wametangazwa kwenye hafla maalum iliyoandaliwa
mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mshindi wa tuzo la mwaka 2014 Yacine
Brahimi, yupo kwenye orodha hiyo pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, André
Ayew, kutoka Ghana, Sadio Mané na Yaya wote wa Ivory Coast.
Mshindi ataamuliwa na mashabiki wa
soka Afrika ambao watapewa fursa kupiga kura hadi tarehe 30, Novemba.
Gharama za matumizi ya simu za
kimataifa itatumika, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako. Ujumbe moja
utatumika kwa nambari moja ya simu pekee.
Mshindi atatangazwa Ijumaa ya
Disemba 11 mwaka huu wakati wa matangazo maalum kwenye BBC World News na BBC
World Service, wakati mitandao ya BBC Sport na BBC Africa ikitoa pia matangazo.
Wagombea wa tatu mwaka huu
waliopigiwa kura na wanahabari 46 kutoka Afrika wamewahi kushinda tuzo hiyo ni Ayew (2011), Touré (2013) na Brahimi (2014).
0 comments:
Post a Comment